Uchunguzi wa Kuyaondoa Mabomu mkoani Okinawa
Simulizi yetu ya leo inatokea kusini-magharibi mwa Japani, mkoani Okinawa. Wakati wa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia, mkoa wa Okinawa ulikuwa eneo la vita vya kutisha vya ardhini. Tani 200,000 za mabomu yalidondoshwa hapo. Hata sasa, takribani mabomu yaliyokosa kulipuka 60,000, yanapatikana Okinawa kila mwaka. Inasemekana kwamba itachukua takribani miaka 70 ili kuyaondoa yote. Mwanamume mmoja amejitolea maisha yake kutafuta mabomu ambayo bado yamefunikwa ardhini. Tulifuatilia kazi ya mwanamume huyu anayesema, miaka arobaini tangu aanze uchunguzi wake wenye mateso.
Takribani mabomu yaliyokosa kulipuka 60,000, yanapatikana Okinawa kila mwaka.
Kabla ya ujenzi wowote wa umma kuanza Okinawa, uchunguzi wa kutumia sumaku unapaswa kufanyika.
Sunagawa Masahiro ni mtaalam wa uchunguzi wa kutumia sumaku.
Mkoani Okinawa, baada ya vita kumalizika, inadhaniwa kuwa takribani tani 10,000 za mabomu yaliyokosa kulipuka yamebaki ardhini. Zaidi ya watu 700 wameathiriwa na mabomu hayo.