Kijiji Kidogo chenye Mawazo Makubwa
Katika kipindi hiki, tunakiangazia kijiji cha Kosuge mkoani Yamanashi kilicho na wakazi wapatao 700. Kijiji hiki kidogo, kinachopatikana tu magharibi ya Tokyo, kinavutia nadhari ya watu wengi nchini Japani. Kimejenga nyumba ndogo lakini unamoweza kuishi kama njia ya kuwachochea vijana kuhamia kijijini hapo. Kijiji hicho ni kidogo, lakini kimechangamka na daima kipo tayari kukabiliana na changamoto mpya. Kinaongozwa na meya Funaki Naoyoshi. Tulimfuatilia meya huyo mchapa kazi.
Funaki alizaliwa na kulelewa kijijini Kosuge. Baada ya kustaafu kutoka kwenye ofisi ya manispaa ya kijiji hicho akiwa na umri wa miaka 52, aligombea umeya wakati wa uchaguzi wa 2012, akilenga kuhakikisha yeyote anaweza akaishi kijijini hapo.
Mradi wa Nyumba Ndogo ulizinduliwa 2016 kwa lengo la kuandaa shindano kila mwaka ambapo washiriki kutoka kote nchini Japani wanapendekeza michoro ya nyumba.
Yeyote anakaribishwa kuzuru chumba cha meya. Funaki amekuwa akijibidiisha kukistawisha kijiji hicho kwa kusikiliza kwa makini maoni na mawazo ya wakazi.