Kutamani Kuguswa na Wapendwa
Janga la virusi vya korona limevilazimu vituo vingi vya kuwatunza wazee kuweka vizuizi vya ziara kati ya wakazi na familia zao. Wanatakiwa hata kutogusa mikono ya wapendwa wao. Tunakuletea simulizi ya familia mbili zinazoendelea kuwa na matumaini licha ya hali ngumu. (Kipindi hiki kilitangazwa Mei 3, 2022.)
Kaskazini mwa Japani, kwenye kituo cha kuwatunza wazee mjini Sendai mkoani Miyagi, mkazi wa kituo hicho anakutana na watoto wake wakubwa. Wakazi na wageni wanaweza tu wakazungumza kupitia kwenye kioo kwa hadi robo saa.
Mkazi anayeugua anakutana na wanawe wa kiume kupitia sehemu zilizotengwa kwa karatasi ya plastiki. Ni familia tu za wakazi wanaokaribia kufa wanaokubaliwa kwenye vyumba baada ya kufanyiwa ukaguzi mkali wa afya.