Mafunzo ya Maisha kutoka kwa Wasiokuwa na Makazi
Simulizi kutoka mjini Kitakyushu mkoani Fukuoka kusini magharibi mwa Japani. Vijana wanajihusisha katika shughuli za kuwasaidia wasiokuwa na makazi mjini humo. Wao ni wanachama wa Hoboku, shirika lisilokuwa la kujipatia faida ambalo limekuwa likitoa usaidizi kwa kipindi cha miaka 33 iliyopita. Kipindi hiki kinabaini namna vijana na watu wasiokuwa na makazi walivyokuza uhusiano unaovuka mipaka ya uhusiano wa kawaida kati ya wanaosaidia na wanaosaidiwa.
Hanaoka Makoto mwenye umri wa miaka 28 akipeana chakula kwenye mvua.
Taguchi Yuzurimwenye umri wa miaka 30 anaizuru mitaa wakati wa usiku. Anasema alisaidiwa na mwanamume aliyekutana naye akiwa mwanafunzi wa shule ya sekondari ya juu, binafsi akikabiliwa na changamoto za mahusiano.
Okuda Tomoshi ni kasisi na mwasisi wa Hoboku. Amewasaidia zaidi ya watu 3,600 wasiokuwa na makazi kutafuta njia za kujipatia kipato.
Nishihara Nobuyukihakuwa na makazi awali. Anawatembelea watu maskini katika jamii na kuzungumza nao kila mwezi.