Kutafuta Amani na Baba Yangu
Tunakutana na Kuroi Akio, mwanamume anayesema daima alimchukia babake. Babake aliyerejea kutoka Vita Vikuu vya Pili vya Dunia alifadhaika. Alikumbana na nini vitani? Miaka 31 baada ya kifo cha babake, tulimfuata Akio msimu mmoja wa joto akiwa katika harakati za kufahamu makovu ya kihisia yaliyosababishwa na vita.
Kuroi Akio mwenye umri wa miaka 72 anazuru kaburi la babake. Uhusiano wake na babake ambaye ni mwanajeshi wa zamani, ulimtatiza.
Kuroi alianzisha sehemu ya familia za wanajeshi wa zamani kutangamana. Nyaraka mbalimbali za wanajeshi hao wenye makovu yaliyosababishwa na vita zinaoneshwa hapo.
Video ya marehemu baba wa Kuroi. Akishindwa kuzungumza na wajukuu wake, alisalia kimya huku familia nzima ikizamia kwenye vicheko.
Albamu ya baba wa Kuroi wakati wa siku zake za uanajeshi, ilipatikana nyumbani kwake. Ina picha ambazo Kuroi hakuwahi kuziona.