Kuishi Kando ya Janga
Julai 2020, mkoa wa Kumamoto ulio eneo la Kyushu magharibi mwa Japani ulikumbwa na mvua kubwa mno. Kufurika kwa mto Kuma unaopita maeneo ya mlimani kuliharibu kabisa au kiasi nyumba 4,600 na watu 65 walifariki. Ujenzi mpya unaosuasua unawafanya wakazi kuzidi kutokuwa na uhakika wa mustakabali wao. Kipindi hiki kinaangazia maisha ya watu kwenye maeneo yaliyoathiriwa. (Kipindi hiki kilitangazwa Februari 1, 2022.)
Eneo la Konose liliathiriwa zaidi na mafuriko. Wanakijiji zaidi ya 300 bado wanaishi katika makazi ya muda makumi ya kilomita kutoka kijijini hapo.
Mto Kuma una urefu wa kilomita 115. Sehemu kubwa za kingo zake ziliharibiwa na mafuriko.
Wakati asilimia 80 ya wakazi wa Konose wakitumai kujenga tena makazi yao, ofisi ya manispaa imetoa ripoti, ikikadiria muda unaohitajika kutekeleza hatua za udhibiti wa mafuriko wa miaka mitano hadi kumi.