Kuokoa Kumbukumbu za Kabla ya Janga
Tunazuru mji wa Okuma mkoani Fukushima. Mtambo wa Nyuklia wa Fukushima Namba Moja upo katika pwani ya mji huu. Mwaka 2019, amri za uhamaji ziliondolewa katika maeneo yaliyoondolewa mionzi hatari, na maandalizi yanaendelea kuwakaribisha tena wakazi. Wakati mwonekano wa zamani wa mji huo ukitoweshwa, serikali ya eneo imeanzisha mradi wa kuhifadhi vitu vilivyookolewa kutoka kwenye majengo yanayosubiri kubomolewa. (Kipindi hiki kilitangazwa Juni 1, 2021.)
Juhudi za uokoaji na uhifadhi wa vitu vya kihistoria zilianza mwaka 2017. Katika "eneo lililo gumu kurejea," kwanza wanahakikisha mionzi ipo chini ya viwango stahiki.
Vitu vilivyookolewa vinahifadhiwa kwenye ukumbi wa mazoezi ya viungo wa mji huo usio na mionzi hatari. Vitu zaidi ya 900 vimekusanywa kutoka kaya za watu na majengo ya umma.
Timu ya uokoaji inaundwa na wakazi wa mji huo waliofika hapo kutoka maeneo mbalimbali ya mkoa huo walikohamia. Katika mji wa Okuma, kaya zaidi ya 1,500 zilikumbwa na uwezekano wa kuachia ardhi iliyomilikiwa na familia zao kwa miaka mingi.