Kuwepo Kwa Ajili ya Wagonjwa wa Kigeni
Mjini Narita, Mkoani Chiba, Mashariki ya Tokyo, kuna hospitali moja inayotembelewa na wagonjwa wengi wa kigeni. Mwaka 2019, ilitembelewa na zaidi ya wagonjwa 4,500 kutoka zaidi ya nchi na maeneo 50. Wengi wa wagonjwa hao wana matatizo – huenda wapo nchini Japani kinyume cha sheria au pengine hawawezi kugharamia malipo yao ya matibabu. Daktari Asaka Tomomi anafanya kazi kama afisa mkuu wa ushirikiano wa wagonjwa wa kigeni hapa. Anafanya kadiri awezavyo kuhakikisha watu wenye mahitaji wanatibiwa. Tunamfuatilia anapotafuta suluhisho licha migogoro iliyopo. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 5, 2019.)
Asaka, daktari anayewatibu wagonjwa wa kigeni walio na wasiwasi katika nchi ya kigeni kwa shauku kuwa "Ikiwa tungekosa kuwahudumia, nani angewahudumia?".
Daktari Asaka Tomomi anafanya kazi kama afisa mkuu wa ushirikiano wa wagonjwa wa kigeni.
Tomomi anataka kuwepo kwa ajili ya wagonjwa anaowahudumia. Lakini dhamira hiyo pekee haitoshi. Inabidi akabiliane na ukweli wa mambo.