Nyumba ya Pamoja, Maisha ya Pamoja
Tunakuletea simulizi kutoka mkoani Fukuoka, eneo la Kyushu magharibi mwa Japani. Hatake no Ie, yaani "Nyumba ya Mashambani," ni nyumba ya kuishi pamoja watu wenye ulemavu, kitu ambacho ni nadra Japani. Wakazi wote wanne ambao ni vijana wana ulemavu mkubwa unaowasababishia kikwazo cha hata kuwasiliana na kuhitaji msaada endelevu. Kipindi hiki kinafuatilia maisha ya wakazi hao wanne na watu wanaowapatia msaada. (Kipindi hiki kilitangazwa Novemba 30, 2021.)
Mizuno Hikari ameishi kwenye "Nyumba ya Mashambani" kwa miaka miwili. Akiugua ugonjwa wa kukakamaa misuli, ameishi nyumbani na hospitalini kwa muda mrefu na kutangamana na watu wengine kwa nadra.
Baba wa Hikari aliongoza jitihada za kufungua "Nyumba ya Mashambani." Alilenga kutengeneza mahali ambapo watu watakutana na kufanya jambo fulani bora.
Wanawake kutoka mitaa jirani hufika hapo kabla ya chakula cha mchana. Wafanyakazi hao wa kujitolea wanaolipwa, wanaoitwa "wahudumu," hufanya kazi kwa zamu kila siku, kama vile kupika na kufua.
Fukagawa Yusei ndio tu amehamia hapo. Kukutana na watu wengine kunahamasisha ukuaji binafsi wa wakazi hao wanne.