Nguvu ya Kukata Tamaa
Tunamwangazia Deguchi Haruaki, Rais wa Chuo Kikuu cha Asia Pasifiki cha Ritsumeikan. Deguchi ana historia ya kipekee kama rais wa chuo kikuu, ikiwemo kuanzisha kampuni akiwa na umri wa miaka 60. Kutokana na virusi vya korona, amekuwa akipata mialiko mingi kutoka kwa majarida na pia ya kutoa mihadhara. Ana wafuasi zaidi ya 130,000 kwenye mitandao ya kijamii. Kwa nini watu wengi wanasaka maneno ya Deguchi? Tunaangalia kwa karibu haiba yake. (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 31, 2021.)
Deguchi Haruaki alipendekezwa kuwa Rais wa APU mwaka 2018.
Rais wa APU Deguchi akiwa na wanafunzi. Karibu nusu ya wanafunzi chuoni hapo ni wa kigeni. Wengi wao wanakabiliwa na hali ngumu kwa sababu ya janga la virusi vya korona.
Kusoma ni chanzo cha maarifa ya Deguchi. Ameshawishiwa pakubwa na kitabu cha Charles Darwin cha "On the origin of Species," alichokisoma akiwa chuo kikuu.