Sushi kutoka Moyoni
Kuna mpishi mkuu nguli wa sushi mjini Kanazawa mkoani Ishikawa, katikati mwa Japani. Morita Kazuo ana umri wa miaka 89 na bado anajishughulisha na upishi wa sushi. Anawavutia wateja kutokana na ujuzi wake wa kutumia kisu, akikata sushi kwa umbo sahihi kutokana na tajiriba ya zaidi ya miongo saba. Kaulimbiu yake ya msingi ni ukarimu. Wakati huu, tunakujuza siri na falsafa za mpishi huyo hodari wa sushi.
Sushi iliyoandaliwa na viambato vilivyochaguliwa kutoka kote nchini.
Mpishi mkuu wa sushi Morita Kazuo anaweza kutambua ubora wa minofu anapoikata kutokana na mguso wa kisu chake.
Kaunta iliyopo jikoni ya umbo la L imetengenezwa ili Morita aweze kutayarisha na kupeana sushi bila kuwapiga mgongo wateja wake.
Morita anatumai vijana wake wakurufunzi wataelewa maana ya kutayarisha sushi kutoka moyoni.