Masomo ya Mwisho ya Mpishi Nguli
Leo tunatembelea sekondari ya juu ya umma mkoani Mie, magharibi mwa Japani. Shule hiyo inafahamika kwa kilabu chake cha upishi wa kitaalam kiasi, kikiongozwa na Murabayashi Shingo anayefahamika mno katika ulimwengu wa mapishi duniani kutokana na mbinu zake sahihi na adilifu za kutoa mafunzo. Baada ya miaka 25 ya kukisimamia kilabu hicho, amepangiwa kustaafu. Kwa mara ya mwisho, yeye pamoja na wanafunzi wake watatayarisha Osechi, chakula cha kitamaduni cha Kijapani cha kusherehekea mwaka mpya. (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 3, 2021.)
Kasha la Osechi lililotayarishwa na wanafunzi wa kilabu cha upishi cha sekondari ya juu mkoani Mie. Shule hiyo hutoa kozi ya upishi.
Murabayashi, mwalimu mkali, anawafunza wapishi wakuu vinara duniani ili kufanya kazi katika hoteli na migahawa ya kifahari kote Japani.
Kilabu cha upishi cha shule hiyo kilianzishwa na Murabayashi kwa ajili ya wanafunzi waliotaka kuwa wataalam zaidi.