Changamoto ya Daktari wa "Ostomate"
Tunakuletea simulizi kumhusu daktari mbobezi Emma Otsuji Pickles mwenye umri wa miaka 42. Baada ya kuugua ugonjwa uliokuwa sugu kutibika, sasa ana "stoma," upasuaji unaofanyika kuunda tundu kwenye ukuta wa tumbo. Hivi karibuni, Emma alishiriki upigaji picha akiwa amevalia bikini, akionesha mfuko wake wa stoma. Hatua yake iliwatia moyo watu wenye hali kama yake. Tutafahamu kilichomfanya kupozi mbele ya kamera.
Tangu alipobalehe, Emma amekuwa akienda na kutoka hospitalini kwa zaidi ya mara 20, kwa sababu mwili wake haukuweza kumeng'enya chakula wala kupitisha kinyesi. Alikuwa na umri wa miaka 38 alipobaini aliugua ugonjwa mgumu kutibu na alikuwa na ogani za kumeng'enya chakula zilizofanya kazi kwa taabu.
Emma anazurukampuni pekee inayotengeneza mifuko ya stoma nchini Japani. Akitumai kuongeza uelewa wa ugumu wanaokabiliwa nao waathiriwa wa hali hiyo, anaamua kuvua jaketi lake na kuonesha mfuko huo.
Upigaji picha wa Emma ulionekana katika kipindi cha runinga na kuchochea mwitikio mkubwa. Waathiriwa wengi na familia zao walituma maoni yao.