Ndoto Imerejelewa
Simulizi kuhusu watu, simulizi kuhusu maisha. Kipindi cha Simulizi za Miji ya Nyumbani kinaelezea uhusiano wa karibu wa watu kutoka kote Japani. Wavuvi wazoefu wanashindana kupata samaki tuna wa mapezi ya buluu mjini Oma, kaskazini mwa Japani, mji wa uvuvi maarufu kwa samaki tuna wake waitwao Oma maguro. Mvuvi limbukeni mwenye umri wa miaka 57 alihamia hapo miaka minne iliyopita akitokea magharibi mwa Japani. Ameamua kufukuzia ndoto yake ya kuwa mvuvi wa samaki tuna baada ya mabinti wake kukua. Baada ya kufanya uamuzi wake wa wapi na jinsi gani ya kuvua, analenga kupata samaki wa mapezi ya buluu wenye uzito wa zaidi ya kilo 100. Tunaifuatilia safari yake ya uvuvi akipambana katika maji ya kaskazini yenye mawimbi tele. (Kipindi hiki kilitangazwa 04 Agosti, 2020.)
Sakamoto Masaoki, mvuvi limbukeni mwenye umri wa miaka 57
Sakamoto Masaoki aliyefukuzia ndoto kwa zaidi ya miaka 50 anaishi katika mji wa uvuvi wakati wa msimu wa samaki tuna hao na kupiga makasia baharini akisaka samaki hao wenye bei ghali watakaomfanya kuwa tajiri mara moja.
Samaki tuna wa mapezi ya buluu wanaovuliwa Oma, mkoani Aomori wanatajwa kuwa ni wa kifahari na wanagharimu hadi yeni milioni 5 au kama dola 45,000 kila mmoja.