Simulizi ya Geiko Mkoani Nara
Simulizi kuhusu watu, simulizi kuhusu maisha. Kipindi cha Simulizi za miji ya nyumbani kinaangazia taswira za karibu za watu kutoka kote Japani, kila moja ikizungumzia maisha tofauti huku iking'arisha maisha ya wengine. Wakati huu kipindi hiki kitazungumzia geiko mkoani Nara, mji wa kale uliopo magharibi mwa Japani. Geiko, ama geisha kama wanavyoitwa katika eneo la Kansai ikiwa pamoja na Nara, ni wanawake wanaoburudisha wateja kwa kutumbuiza nyimbo za kitamaduni, dansi na kupiga ala ya shamisen.Tunamulika maisha ya geiko mmoja wa Nara aitwaye Kikuno, ambaye anapambana kurithisha utamaduni huo kwa vizazi vijavyo.
(Kipindi hiki kilitangazwa Julai 7, 2020.)
Kikuno amekuwa akifanya kazi kama geiko mkoani Nara.
Kikuno (kushoto) anawafunza vijana ujuzi aliojifunza kutoka kwa watangulizi wake.
Kikuno (katikati) akitumbuiza jukwaani pamoja na vijana wake.