Mapito ya Nyakati Ngumu
Tunawatembelea wanachama wa kampuni ya mabasi ya kukodi iliyoathiriwa mno na COVID-19. Wakuu wa kampuni hiyo walilazimika kufanya uamuzi mgumu wa kuwafuta kazi wafanyakazi kadhaa. Na wale waliosalia kazini walilazimika kutafuta namna ya kujikimu baada ya mishahara yao kupunguzwa. Kwa miezi sita, tuliwafuatilia katika mahangaiko yao. (Kipindi hiki kilitangazwa Disemba 1, 2020.)
Kampuni ya kukodisha mabasi yenye makazi yake mkoani Fukuoka. Makundi ya watalii kutoka China yaliyochangia karibu asilimia 40 ya mapato, yalikuwa yote yamefuta ziara yao.
Afisa mkuu mtendaji Kaieda Tsukasa amekuwa akizipigia simu benki siku baada ya siku akijaribu kutafuta fedha. Wafanyakazi waliosalia kazini wanaendelea kufanya kazi za muda mbali na kazi hiyo ili kusaidia familia zao.
Dereva Nakagawa Kaori anaangazia huduma zingine zinazoweza kutolewa na kampuni hiyo, ili kufidia ziara za kitalii zilizopungua.