Mhimili wa Wabrazil nchini Japani
Idadi ya raia wa kigeni mjini Izumo mkoani Shimane imeongezeka kwa kasi kwa sababu ya mipango ya upanuzi wa viwanda vya uzalishaji.  Mzozo wa China na Marekani  uliathiri biashara na mapato ya wafanyakazi yaliporomoka. Lakini kuna mtu wa kumtegea. Anajulikana kama Paizão, yaani  "big daddy," ni Mbrazil mwenye asili ya Japani aliyeishi Japani kwa karibu miaka 30. Fuatilia jitihada za mtu mmoja asiyechoka kujenga daraja la kudumu kati ya Brazil na Japani.
Takinami Sergio, maarufu kama Paizão, yaani "Big Daddy." (kulia)
Mbali na kuendesha mgahawa wa Kibrazili na Shirika lisilo la kujipatia faida, Paizão anajitoa kusaidia marafikize Wabrazil na kuimarisha maelewano ya pande mbili kati yao na Wajapani.
Familia ya Yendo Fabio aliyepoteza kazi yake kiwandani na kuhitaji kazi nyingine. Walihamia Izumo miaka 4 iliyopita akitumai kuendelea kuishi hapo.
Baada ya miezi 6 ya kusaka kazi bila mafanikio, Yendo Fabio aliamua kuondoka Japani. Paizão alishuhudia kuondoka kwa familia zaidi ya 10.