Jack Sim / Mwasisi wa WTO, Shirika la Choo Duniani, Almaarufu Bwana Choo
Watu wapatao milioni 2 duniani wanasemekana kutokuwa na vyoo bora na usafi. Katika nchi zinazoendelea, ukosefu wa vyoo unasababisha magonjwa na uchafuzi wa maji kuenea, na hata kusababisha vurugu na unyanyasaji dhidi ya wanawake. Mjasiriamali wa kijamii wa Singapore Jack Sim amekuwa akijibidiisha kulikabili suala hili la afya ya umma. Mwasisi huyo wa Shirika la Choo Duniani anazungumzia jitihada zake za kukabiliana na suala hili linalochukuliwa kuwa mwiko katika jamii.
Jack Sim / Mwasisi wa WTO, Shirika la Choo Duniani, Almaarufu Bwana Choo.