Roboti ya Kuokoa Kilimo
Idadi kubwa ya wazee na upungufu wa wafanyakazi ni moja ya masuala makubwa yanayoikumba kwa sasa sekta ya kilimo nchini Japani. Katika kipindi hiki, tunakutana na Tamir Blum, mvulana wa Kiisrael ambaye anafanya kazi ya kupunguza mzigo kwa wakulima wa Japani kwa kutumia roboti! Kutoka katika ofisi yake iliyopo mkoani Chiba, yeye na timu yake wanaendeleza roboti ambayo anaamini itawasaidia wakulima duniani kote kwa kazi zinazohitaji kufanywa na mwili wa binadamu. (Kipindi hiki kilitangazwa Machi 7, 2023.)
Tamir Blum anatoka nchini Israel.
Anaendeleza roboti ya kufanya kazi za kilimo inayoendeshwa kwa mfumo wa AI.
Kwa kutumia teknolojia ya kifaa kinachotembea juu ya uso wa dunia, roboti hiyo imeundwa kwa ajili ya kazi kama vile kubeba mazao yaliyovunwa.
Akaishi Jun-ichi (upande wa kulia kabisa) anaanda shamba lake la tufaha ili kujaribu roboti. Na Tamir (upande wa kushoto kabisa).