Kulima Vito Ving'aavyo Vyenye Ladha
Katika kipindi hiki, tumeelekea mjini Mitoyo mkoani Kagawa kukutana na raia wa Ufaransa Jérôme Rupp anayelima Shine Muscats, mizabibu ya aina ya kipekee iliyoanzia kulimwa nchini Japani. Kulima matunda hayo ghali ni kazi inayoumiza inayohitaji uangalizi wa kina. Baada ya mafunzo chini ya mshauri, Jérôme hatimaye alivuna zabibu zake za kwanza. Hata hivyo, baadhi ya zabibu hizo zilikuwa zimeharibiwa na kimbunga. Je matunda ya kazi yake yatakuwaje msimu ujao? (Kipindi hiki kilitangazwa Februari 7, 2023.)
Mzaliwa wa Ufaransa Jérôme Rupp alianzisha shamba lake miaka mitano iliyopita. Mwaka 2021, alivuna mizabibu kwa mara ya kwanza.
Jérôme alijifunza kazi ya kulima mizabibu kutoka kwa mshauri wake, Yano Yasue.
Familia ya Jérôme inaendesha duka la vitamutamu katika eneo wanaloishi. Huku msimu wa mavuno ukikaribia, Jérôme anamuda mchache wa kukaa na familia yake.
Wakati mji huo ukikosa wafanyakazi vijana na wakulima wakizeeka, Jérôme ana jukumu la kufikia matarajio ya jamii.