Mwanzo Mpya kwa Mfugaji Ng'ombe Mzee
Katika kipindi hiki, tumekutana na mzaliwa wa Marekani Tim Jones anayeishi mji wa Kuromatsunai mkoani Hokkaido. Tim ni mfugaji mkongwe kutoka Texas, alikuwa na umri wa miaka 68 wakati ambapo yeye na mke wake Mjapani walipoamua kuhamia nchini Japani miaka miwili iliyopita ili kufuga ng'ombe. Je Tim ataweza kuuza nyama ya ng'ombe wasio na kiasi kikubwa cha mafuta waliolishwa kwa nyasi nchini Japani ambapo watu wanathamini nyama yenye mafuta. (Kipindi hiki kilitangazwa Januari 10, 2023.)
Tim alianzisha shamba la kufugia ng'ombe mjini Kuromatsunai mkoani Hokkaido.
Shamba lililotelekezwa limebadilishwa na kuwa malisho bila kutumia kemikali za kilimo.
Tim alianzisha maelekezo ya kufuga ng'ombe wanaolishwa nyasi kwa kushirikiana na watu wa eneo hilo.
Tim aliuza nyama ya ng'ombe waliozalishwa nchini Japani kwa mara ya kwanza wakati wa msimu wa baridi mwaka 2022.