Kukuza Mustakabali wa Uvuvi
Nakanoshima ni sehemu ya mtungo wa visiwa vya Oki vilivyoko katika Bahari ya Japani. Raia mmoja wa kigeni anafanya kazi katika sekta ya uvuvi iliyostawi kisiwani hapo tangu zamani. Aung Moe Oo anatokea Myanmar. Tunafuatilia jitihada zake za kurithisha vizazi vijavyo uvuvi katika kisiwa hicho. (Kipindi hiki kilitangazwa Julai 5, 2022.)
Aung Moe Oo amekuwa mvuvi katika eneo la Nakanoshima kwa miaka 17. Kwa sasa anaongoza timu ya watu 11.
Wavuvi wote 12 katika timu yake, akiwemo Aung Moe Oo, wanatoka nje ya Nakanoshima. Wengi wao walikuwa wakifanya kazi zingine.
Hamaguchi Natsuki (Kushoto) ameanza mafunzo ya uvuvi. Alihitimu shule ya muziki jijini Tokyo na kufundisha upigaji piano wakati akiifanyia kazi kampuni moja ya Teknolojia ya Habari kabla ya kuja kisiwani hapo.