Kuhudumia Supu ya Nyoka wa Ryukyu
Katika kipindi hiki, tumetembelea kijiji cha Kitanakagusuku kilichopo mkoani Okinawa kukutana na mzaliwa wa Marekani, Alex Hopson ambaye anafanya kazi katika mgahawa unaohudumia supu yenye aina ya viambato vikuu vya kipekee vya nyoka wa baharini mwenye sumu kali! Ni mlo ambao umekuwa ukitumika tangu Ufalme wa Ryukyu ulipokuwa ukitawala kisiwa cha Okinawa. Alex amekamilisha dhamira yake ya kutunza supu hii ya kipekee na utamaduni wa mapishi wa eneo hilo. (Kipindi hiki kilitangazwa Desemba 6, 2022.)
Alex, akiwa amebeba irabu waliokaushwa kwa moshi
Supu ya irabu (irabu=nyoka wa baharini wenye sumu kali)
Alex, mkewe Izumi, na mama mkwe Fujiko
Alex akifanya mkutano kwa njia ya mtandao na moja ya kampuni jijini New York