Kantini ya Watoto ya Tony Yafika Barabarani
Katika kipindi hiki, tunamtembelea tena mzaliwa wa Ghana, Tony Justice, ambaye anaendesha kantini kwa ajili ya watoto kutoka familia zisizo na uwezo wa kifedha na kaya zenye mzazi mmoja katika Mkoa wa Kanagawa. Akitafuta kuendeleza mradi wake katikati ya janga la virusi vya korona, aliamua kuingia barabarani! Akiwa na lori la chakula, aligeuza mlo wa jioni kufanyika katika kantini inayotembea maeneo ya nje. Tunaambatana na Tony anayejitayarisha kupeleka kantini yake inayotembea jijini Tokyo!
Lori la chakula la Tony Justice likiwa barabarani.
Kwa kufungua kantini ya nje kwa watoto wenye uhitaji, Tony anaandaa chakula cha Kiafrika aina ya supu nyepesi ya nyanya ndani ya lori lake la chakula.
Tony Justice anatokea nchini Ghana.