Safari ya Sanaa ya Mapigano kwa Mvulana wa Kiukraine
Shujaa wa kipindi hiki ni mvulana raia wa Ukraine Artem Tsymbaliuk mwenye umri wa miaka kumi na mitatu, mwanafunzi wa sanaa ya mapigano kwenye dojo moja iliyopo kwenye mji wa Takamori uliozungukwa na milima yenye urefu wa zaidi ya mita 2,000, mkoani Nagano. Artem ni miongoni mwa watoto kutoka familia nne za Kiukraine waliokuja nchini Japani kutafuta hifadhi, kufuatia uvamizi wa Urusi nchini kwao. Dojo kuu ya Takamori iliwapokea watoto hao. Hii hapa ni simulizi ya Artem, mwanamichezo chipukizi wa sanaa ya mapigano aliyekimbia vita akiwa na mama yake.
Artem Tsymbaliuk mwenye umri wa miaka kumi na mitatu kutoka nchini Ukraine, akifanya mazoezi ya sanaa ya mapigano katka dojo.
Artem Tsymbaliuk kutoka Ukraine na mama yake, Olena Volosenko.
Artem na Ozawa Takashi ambaye ni mwenyekiti wa Zendokai Karate aliyewakaribisha wanafunzi kutoka Ukraine.