Kuishi na Msitu na Mlima
Chini ya milima ya Alps Kaskazini mwa mkoa wa Nagano upo mji wa Matsumoto. Mzaliwa wa Nepal Lama Gyalu, ambaye anatokea maeneo ya mlima wa Sherpa uliopo Tibet, anafanya kazi ya kulinda mazingira asilia ya milima katika eneo hilo. Anatumia ujuzi alioupata katika kazi ya kuongoza watu milimani katika nchi yake ya nyumbani, kwa kutumia njia maalum ya ukataji miti aliyoibuni mwenyewe. Tunamfuatilia katika kazi zake za kila siku. (Kipindi hiki kilitangazwa mnamo Agosti 10, 2021.)
Lama mzaliwa wa Nepal ni mjuzi wa kuongoza watu kupanda milima, ambaye ameshafanya safari nne za kufika kilele cha mita 8,000.
Nagano ni moja ya sehemu nchini Japani iliyokumbwa na wadudu tishio kwa misitu hususani mbao za misonobari wanaoitwa nematodi. Ili kujilinda na wadudu hao wasisambae zaidi, Lama anakata miti ya misonobari iliyoathiriwa.
Kwanza Lama anakata matawi yaliyochipuka na anaendelea taratibu kukata shina vipande vipande, hivyo anapunguza uharibifu kwa miti iliyo karibu.
Lema anaishi na mke wake Mariko pamoja na watoto wake wawili wa kiume.