Hakuna Aliyeachwa Nyuma
Tunamtembelea mkimbizi kutoka Myanmar Aung Myat Win anayeendesha mgahawa uliopo jijini Osaka unaoandaa vyakula vyenye ladha halisi ya nchi yake. Win pia anaendesha biashara ambayo inatoa huduma kwa watu wenye ulemavu. Kwa hali ya sasa ilivyo nchini mwao, Win anatoa usaidizi kwa raia wa Myanmar waliopo nchini Japani ambao wanapitia hali aliyowahi kuwa nayo wakati alipowasili nchini humo miaka 20 iliyopita. (Kipindi hiki kilitangazwa Septemba 6, 2022.)
Aung Myat Win kutoka Myanmar.
Mgahawa wa Win unawavutia wateja Wajapani wenye shauku ya kujaribu ladha za vyakula vya kigeni.
Profesa Suoh Setsuo aliyemsaidia Win.
Win anawasaidia watu kutoka Myanmar wanaosubiri majibu kuhusiana na hadhi yao ya ukimbizi.