Programu ya Kompyuta ya Kuwasaidia Wanawake na Ukraine
Simulizi yetu hii leo inamuangazia Anna Kreshchenko, mwanamke wa Ukraine anayeishi katika mji mkuu wa zamani wa Japani, Kyoto. Alianzisha kampuni binafsi inayoendeleza programu za kompyuta kusaidia afya ya wanawake wakati akiwa mwanafunzi. Kwa sasa, anasaidia watu nchini mwake kutokea nchi ya mbali ya Japani. Hebu tumfuatilie Anna katika jitihada zake za kuwasaidia Waukreni wenzake waliopo nyumbani na wanawake kote duniani. (Kipindi hiki kilitangazwa Agosti 9, 2022.)
Anna Kreshchecnko ni mwanamke wa Ukraine anayeendeleza programu za kompyuta kusaidia afya ya wanawake nchini Japani.
Ivan Seleznov ni mwanzilishi mwenza wa kampuni ya Anna, mwanafunzi wa uzamili anayetafiti uhandisi wa vifaa tiba.
Mtu mmoja alimtaka Anna kumsaidia, naye ni mkimbizi kutoka Ukraine aliyewasili Kyoto hivi karibuni.