Mshonaji Mtogo Ausisimua Mji wa Kyoto
Mshonaji kijana kutoka Afrika anausisimua mji wa Kyoto, ambao ni kitovu cha vitambaa vya kitamaduni vya Kijapani. Kabressa Deabalo mwenye umri wa miaka 30 anaitwa mshonaji mahiri katika nchi yake ya nyumbani ya Togo. Tunakusimulia jitihada zake za kunadi ujuzi wake wa Kiafrika katika uliokuwa mji mkuu wa Japani, Kyoto. (Kipindi hiki kilitangazwa Oktoba 12, 2021.)
Mshonaji mzawa wa Togo, Kabressa Deabalo.
Jaketi linalojumuisha kitambaa cha kitamaduni cha Kyoto na ujuzi wa Deabalo.
Mtiaji rangi mjini Kyoto anayerithi ujuzi wa kitamaduni (kulia). Deabalo alivutiwa na mbinu yake ya kisasa.
Deabalo alikutana na Nakasu Toshiharu (kushoto), Mjapani aliyehangaika kuunganisha mji wa Kyoto na Togo kupitia vitambaa. Wawili hao walifungua duka lao la kushonea nguo.