Kuvipa Visu vya Kijapani Sura Mpya
Sanaa ya kitamaduni ya Kijapani ya unoaji visu imebadilika hadi kuanza kutumia ujuzi wa kisasa wa kunoa visu vya upishi. Visu mbalimbali vimetengenezwa kulingana na aina ya vyakula, na kuchangia ubora na mvuto wa vyakula vya Kijapani. Aanayetekeleza wajibu katika kuvinadi visu vya Kijapani ni Bjorn Heiberg kutoka Canada, anayeendesha duka lake nchini Japani. Tunafuatilia juhudi za Bjorn za kunoa utamaduni wa Japani wa unoaji visu.
Akivutiwa na visu vya upishi vya Japani, Bjorn alipata mafunzo kwenye mtengenezaji wa visu kabla ya kufungua duka lake mwenyewe 2011. Linauza visu vya upishi kutoka kote Japani.
Visu vya Kijapani vilivyotengenezwa kwa kutumia ujuzi wa kitamaduni. Ukingo ulionolewa barabara unakata vizuri zaidi.
Bjorn anajichukulia kama "mshauri wa visu," anayewaunganisha watengenezaji na wateja. Hususan, hujitahidi kuwasilisha wanachokitaka wateja kwa wasanii.
Bjorn alizuru mji wa Seki mkoani Gifu unaofahamika sana kwa kutenegeneza visu vizuri. Alimtaka Kobayashi Hiroki, fundistadi anayechipukia kumtengenezea kisu kipya. Visu vya Kobayashi vinapendwa mno na baadhi ya wapishi wakuu.