Madaktari wa Wanyama kutoka Vietnam na Farasi wa Hokkaido
Urakawa kusini mwa Hokkaido, iliyopo kaskazini mwa Japani ni eneo ambako farasi wa mbio hufugwa na kufunzwa. Hapo, mashamba karibu 150 yanakuza farasi wa mbio tarajali zaidi ya 1,300 kila mwaka. Lakini miaka ya hivi karibuni, wafugaji wanakumbwa na uhaba wa wafanyakazi. Bao na Hieu wamefika hapo kutoka Vietnam, na kuajiriwa na shamba lililoajiri wahudumia farasi. Tuwafuate katika jitihada zao za kila siku. (Kipindi hiki kilitangazwa Julai 6, 2021.)
Nguyen Van Bao mwenye umri wa miaka 24 (kushoto) na Nguyen Van Hieu mwenye umri wa miaka 33 (kulia). Ingawa walifahamu kidogo tu juu ya farasi awali, wanajibidiisha kuwa wakuzaji bora wa farasi wa mbio.
Shamba hili limebobea katika uzalishaji na ukuzaji wa farasi kabla ya kupewa mafunzo ya mbio.
Bao na Hieu wanaishi nyumba moja iliyopo shambani hapo. Wote ni madaktari wa wanyama waliothibitishwa. Lakini hawakuweza kuzungumza Kijapani kabisa.