Utengenezaji wa Pombe ya Sake
Kutoka enzi za zamani, eneo lililopo kaskazini ya Ziwa Biwa, ziwa kubwa zaidi nchini Japani, limezalisha sake tamu, likitumia maji ya chini ya ardhi na mchele wa eneo hilo wa ubora wa hali ya juu. Kipindi hiki kinamwangazia Enrico Cupri, raia wa Italia aliyejitolea kutengeneza sake tamu kwenye kampuni moja ya kutengeneza pombe iliyoasisiwa karibu miaka 400 iliyopita.
Enrico Cupri alianza kutengeneza pombe ya sake miaka mitatu iliyopita. Anaielezea sake kama "kinywaji kinachogusa moyo na roho."
Enrico anapewa mafunzo ya usuuzaji wa mchele, hatua ya kwanza katika utengenezaji wa sake. Kuelewa mchele ni msingi wa utengenezaji wa pombe hiyo. Wakati wa kuuacha mchele unyonye maji unabadilishwa kulingana na halijoto au aina ya mchele.
Enrico anashiriki utengenezaji wa pombe wa mwaka huu. Katika chumba kinachoitwa muro, koji inanyunyizwa kwenye mchele uliovukizwa na kuchachushwa.