Kufurahishwa na Rangi za Gifu
Kipindi hiki kinamzungumzia mzawa wa Ujerumani, Bernd Kestler ambaye ni msanii wa ufumaji. Akiwa na mapambo ya ubunifu na uchanganyaji rangi wa kipekee, kazi zake zimekuwa zikivutia watu na hadi sasa zimechapishwa kwenye vitabu tisa. Kazi ya Bernd, upendo wake kwa mandhari ya Gifu, mkoa uliopo katikati mwa Japani na juhudi zake za kuutangaza mkoa huo.
Bernd Kestler alivutiwa na ufumaji kwa ushawishi wa dadake na kujifunza ujuzi huo mwenyewe akiwa na umri wa miaka 12.
Moja ya kazi za Kestler. Anatafuta njia mpya ya kujieleza ambayo ni zaidi ya wazo la kawaida la ufumaji.
Kestler anatembelea sehemu mbalimbali za mkoa wa Gifu kwa pikipiki na kuchukua rangi za mandhari anayoyapenda kwa ajili ya kuipamba kazi yake.
Pia ameanza kutengeneza nyuzi za kipekee pamoja na karakana ya utiaji rangi.