Nchi Mpya, Maisha Mapya, Ndoto Mpya
Anayemulikwa katika simulizi hii ni Maurice Torralba kutoka Cuba. Anafanya kazi kama msaidizi wa mkufunzi wa mazoezi ya viungo kwenye sekondari ya juu mjini Miyakonojo mkoani Miyazaki, kusini magharibi mwa Japani. Wakati mmoja akiwa mchezaji wa mpira wavu aliyetazamiwa kufanikiwa nchini Cuba, Maurice alilazimika kuachana na taaluma hiyo akiwa kijana, kutokana na ugonjwa mkali wa henia kwenye uti wa mgongo. Baada ya hapo, alioana na mwanamke Mjapani. Sasa, anafuatilia ndoto mpya katika nchi yake ya pili ya nyumbani.
Maurice, aliye na urefu wa sentimita 195, alichaguliwa kuwa mwanachama wa timu ya taifa ya Cuba akiwa na umri wa miaka 16. Timu hiyo ilishinda mashindano ya Amerika Kaskazini na Kati miaka 3 mtawalia.
Akijituma michezoni maishani, Maurice aliasisi falsafa yake ya mafunzo: kamwe hawakasirikii wanafunzi, haijalishi wamekosa nini.
Mkewe, Nahoko, ni daktari wa meno anayependa muziki aina ya salsa. Wawili hao walikutana Nahoko alipoitembelea Cuba.