Chuo Kikuu Kinachokuza Mabadilishano na Utofauti: Rais wa Chuo Kikuu cha Kyoto Seika, Oussouby Sacko
Tunamwangazia Oussouby Sacko, rais wa kwanza wa chuo kikuu nchini Japani kutoka nchi ya Afrika. Amekuwa akijitolea kukuza mabadilishano kati ya wanafunzi Wajapani na wale kutoka ng'ambo ambao idadi yao imekuwa ikiongezeka kutokana na juhudi zake. Hata hivyo, janga la korona linafanya iwe vigumu kwa Sacko kufuatilia ndoto yake ya chuo kikuu kilichofungua milango yake kwa utofauti.
Mwaka 2018, Sacko ambaye ni mzawa wa Mali alishindana na maprofesa wawili Wajapani kwa wadhifa wa urais, na alichaguliwa.
Sacko alikuja Japani mwaka 1991 na kusomea shahada ya uzamili katika chuo kikuu cha Kyoto akitafiti usanifu wa maeneo uliochochea mabadiishano kati ya watu.
Sacko anaamini hakuna kitu kinachoweza kufikia kile tunachojifunza kutokana na tajiriba ya moja kwa moja. Ni kitu alichojifunza kwa kutangamana na wanafunzi.