Jitihada za kila Siku za Muuza Magari ya Mtumba wa Pakistan
Idadi ya watu walioichagua Japani kuwa makazi yao mapya imevunja rekodi ya juu mwaka 2019, ikizidi watu milioni 2.8. Hiyo ni sawa na karibu asilimia mbili ya watu wote nchini humo. Wanaleta tamaduni mpya katika nchi hiyo, lakini bado wengi wao wanapambana kuendana na jamii. Kipindi hiki kinaangazia maisha yao na changamoto wanazokumbana nazo katika jamii ya Japani. Zaidi ya wauzaji 600 kutoka Asia na Mashariki ya Kati wanakusanyika katika mnada mkubwa wa magari ya mtumba. Ni wauzaji wa bidhaa nje ya nchi ambao ni raia wa kigeni waliofika kuishi Japani, wakitafuta shughuli bora na kujaribu kuzifanya kuwa bora katika nchi hiyo waishio sasa. Mpakistani, Mian Mohammad Sadiq ni mmoja wao. Tunaambatana naye katika jitihada zake za kila siku. (Kipindi hiki kilitangazwa Julai 14, 2020.)
Mian Mohammad Sadiq, kutoka Pakistan, ni muuza malori ya mtumba katika mji wa Oyama, mkoani Tochigi.
Sadiq akishindania magari ya mtumba kwenye mnada mjini Oyama.
Waislamu waliojitolea, akiwemo Sadiq, walijenga moja ya misikiti mikubwa zaidi nchini Japani.