Jitihada za Kuhifadhi Shamba la Eneo ~ mkoani Oita, Paul Christie~
Idadi ya watu waliochagua Japani kuwa makazi yao mapya iliweka historia mwaka 2019, ikizidi watu milioni 2.8. Wanachangia mambo mapya kwa nchi, lakini raia wengi wa kigeni wanahangaika kuendana na jamii hiyo. Kipindi hiki kinaangazia changamoto za raia wa kigeni katika sekta ya utalii akijaribu kukabiliana na athari za janga la korona. Tuliandamana na raia huyo Mwingereza anayeratibu ziara za mashambani mkoani Oita huku akifanya juhudi za kuhifadhi mashamba ya eneo hilo.
Paul Christie na familia yake. Paul anaendesha kampuni ya wakala wa safari mkoani Oita.
Mwanamke akimshukuru Paul kwa kumsaidia kupanda mpunga.
Paul akipanda mpunga kwenye shamba lililotelekezwa.