Kupambana ili Kurejesha Hali ya Kawaida katika Sekta ya Migahawa
Kwa sasa, raia wa kigeni wapatao milioni 2.8 ni wakazi rasmi wa Japani, ambao ni sawa na karibu 2% ya idadi ya watu wote nchini humo. Kipindi hiki cha "Tunapopaita Nyumbani," kinamulika maisha na changamoto wanazozikabili katika jamii ya Kijapani. Wakati huu, tumemwangazia binti mmiliki wa mgahawa, Aya Wu kutoka China anayepambana kudumisha biashara yake wakati wa janga la virusi vya korona.
Aya Wu kutoka China anaendesha mgahawa maarufu wa Kichina katika mji wa Kawaguchi, mkoani Saitama.
Chakula cha pilipili cha mtindo wa Sichuan ni miongoni mwa vyakula pendwa kwa wateja wa mgahawa wake Aya.
Aya alijitolea kufanya usafi kwenye mtaa wa eneo lake miaka mitatu iliyopita.
Katika harakati za kufufua mgahawa wake, Aya anajaribu huduma mpya kama vile kuwasilisha chakula kwa wateja.