Riwaya - "Timu ya Ndoto ya Kutafuta Ndoa" na Hiiragi Sanaka: Sehemu ya Kwanza
Fumiko na marafikize wa utotoni Saaya, Ichiko na Eimi. Wamekuwa wakihangaika bila mafanikio kwenye suala la utafutaji wapenzi na kubuni wazo la kuungana kusaka wenza wa ndoa pamoja. Mikakati yao ni kupitisha utaalamu wao binafsi kwa msichana mrembo Eimi na kumfanya kutenda mambo kama mwanamke mkamilifu. Timu hii ya ndoto ya kutafuta ndoa ipo tayari kusaka wenza kwa mara ya kwanza, lakini hali isiyotarajiwa inawasubiri. Tangu alipoanza utunzi mwaka 2013, mwandishi wa vitabu Hiiragi Sanaka ameshatoa kazi nyingi za mafumbo zenye mtindo wa kusisimua moyo zinazowahusisha wahusika waakuu wa kike. Riwaya hii fupi yenye kuchekesha inatumia mifano halisi ya usimuliaji hadithi wenye taswira za urafiki wa wanawake na harakati zinazohusiana na ndoa na mahaba.