Riwaya - Simu ya Dakika 5
"Simu ya Dakika 5" iliyoandikwa na Tachibana Tsubasa.
Mimi ni mwanafunzi wa chuo kikuu aliyechoshwa na simu za usiku wa manane ninazopigiwa na mtu mmoja. Simu hizo mara nyingi hasa huwa zinadumu dakika tano. Mtu huyo mara nyingi hunichokoza. Usiku huu, ninafanya jambo muhimu maishani linalohusu mustakabali wangu. Kipi nitaamua kufanya? Na ni mtu yupi aliye upande wa pili wa simu?