Kifahamu Kijapani
Karibu kwenye kipengele cha "Kifahamu Kijapani kupitia kwenye habari." Katika kipengele hiki, tunajifunza misamiati ya Kijapani kupitia habari. Kichwa cha habari cha leo ni "Watu watumia kifaa cha AED kumwokoa msichana aliyeanguka ghafla kwenye ukumbi wa mazoezi ya viungo", kilichochapishwa kwenye tovuti ya NEWS WEB EASY Mei 19, 2022. Maneno muhimu ni pamoja na 「体育館(たいいくかん)taiikukan」"ukumbi wa mazoezi ya viungo na 「心臓(しんぞう)shinzoo」"moyo".