Kifahamu Kijapani
Karibu kwenye kipengele cha "Kifahamu Kijapani kupitia kwenye habari." Katika kipengele hiki, tunajifunza misamiati ya Kijapani kupitia habari. Kichwa cha habari cha leo ni "Maonyesho ya Nyaraka za Kihistoria Kuadhimisha Miaka 50 Tangu Japani Irejeshewe Okinawa", kilichochapishwa kwenye tovuti ya NEWS WEB EASY Mei 2, 2022. Maneno muhimu ni pamoja na 「公文書(こうぶんしょ)koobunsho」waraka rasmi na「元総理大臣(もとそうりだいじん)motosooridaijin」 Waziri Mkuu wa zamani.