Kifahamu Kijapani
Karibu kwenye kipengele cha "Kifahamu Kijapani kupitia kwenye habari." Katika kipengele hiki, tunajifunza misamiati ya Kijapani kupitia habari. Kichwa cha habari cha leo ni “Shirika la kimataifa laundwa ili kupambana na tovuti ghushi za katuni za Manga na Anime”, kilichochapishwa kwenye tovuti ya NEWS WEB EASY Aprili 11, 2022. Maneno muhimu ni pamoja na 「海賊版(かいぞくばん) kaizokuban 」toleo ghushi na 「著作権(ちょさくけん)chosakuken」 hakimiliki.