Kifahamu Kijapani
Karibu kwenye kipengele cha "Kifahamu Kijapani kupitia kwenye habari." Katika kipengele hiki, tunajifunza misamiati ya Kijapani kupitia habari. Kichwa cha habari cha leo ni "Mvua Isiyokuwa ya Kawaida" inayonyesha "Mara kwa Mara" nchini Japani Inayosababishwa na Halijoto Zinazopanda", kilichochapishwa kwenye tovuti ya NEWS WEB EASY Mei 11, 2022. Maneno muhimu ni pamoja na 「異常な雨(いじょうなあめ) ijyoona ame」"isiyokuwa ya kawaida" na 「中国地方(ちゅうごくちほう)chuugoku chihoo」Eneo la Chugoku.