Kifahamu Kijapani
Karibu kwenye kipengele cha "Kifahamu Kijapani kupitia kwenye habari." Katika kipengele hiki, tunajifunza misamiati ya Kijapani kupitia habari. Kichwa cha habari cha leo ni "Watafiti waendeleza plastiki inayooza baada ya kutumiwa", kilichochapishwa kwenye tovuti ya NEWS WEB EASY Aprili 6, 2022. Maneno muhimu ni pamoja na 「プラスチック(ぷらすちっく) purasuchikku」plastiki na 「ごみ gomi」taka.