Riwaya - Kuondoka: Sehemu 3 / Kifahamu Kijapani
Kutokana na janga la kudorora kwa uchumi duniani, Koichi anakabiliwa na chaguo la kushushwa cheo na kupunguziwa mshahara au kustaafu mapema kutoka kwenye kampuni ambako daima amehudumu. Wakati huohuo, nyumbani kwake, anapaswa kumshughulikia mwanawe wa kiume. Koichi alishikilia mtazamo uliopitwa na wakati kwamba mwanawe alihitaji kuhitimu kutoka chuo kikuu kinara na kufanya kazi kwenye kampuni kubwa. Sasa analikabili pengo lililopo kati yake na mwanawe, ambaye anahitaji kuhimili enzi ya sasa. Koichi atamwambia nini mwanawe, ikizingatiwa kwamba yeye pia anakabiliwa na hatari ya kufutwa kazi? Kwenye "Kifahamu Kijapani," utajifunza maneno mengi ya Kijapani kutokana na habari inayohusu filamu ya 'Drive My Car' iliyoshinda Tuzo ya Academy katika Kipengele Bora cha Kimataifa.
---
Karibu kwenye kipengele cha "Kifahamu Kijapani kupitia kwenye habari." Katika kipengele hiki, tunajifunza misamiati ya Kijapani kupitia habari. Kichwa cha habari cha leo ni "Drive My Car' Yashinda Tuzo ya Academy ya Kipengele Bora cha Kimataifa", kilichochapishwa kwenye tovuti ya NEWS WEB EASY Machi 28, 2022. Maneno muhimu ni pamoja na 「アカデミー賞(あかでみーしょう) akademii shoo」 Tuzo za Academy na 「外国(がいこく) gaikoku」nchi ya kigeni.