Riwaya - Kuondoka: Sehemu 2
Janga la mdororo wa kifedha duniani linaathiri kampuni anayoifanyia kazi Koichi. Anakabiliwa na hatari ya kushushwa cheo na kupunguziwa mshahara au kustaafu mapema katika kampuni ambako daima amehudumu. Wakati huohuo, nyumbani kwake, anahitaji kuwazia cha kufanya kumhusu mwanawe, aliyefilisika na hana ajira. Awali, alimuita mwanawe "mshinde," lakini sasa yeye mwenyewe anakabiliwa na hatari kufutwa kazi, na anajiuliza ni vipi atakavyomkabili mwanawe. Nini kitatokea nyumbani kwake Koichi?