Riwaya - Kuondoka: Sehemu 1
Alfajiri moja, mhusika mkuu Koichi anampata mwanamume mmoja akiwa ameanguka kwenye mlango wake wa mbele. Ni mwanawe wa kiume Ryoji, ambaye alikuwa mbali na familia yake kwa miaka 5. Mkewe Akiko anahofia afya ya Ryoji, lakini Koichi anamuita "mshinde." Koichi anavunjwa moyo na mwanawe ambaye hakwenda chuo kikuu au kupata kazi kwenye kampuni kubwa, na amerudi nyumbani akiwa katika hali mbaya. Kisha Koichi anaitwa katika mkutano wa dharura wa kampuni huko kazini.