Kifahamu Kijapani
Karibu kwenye kipengele cha "Kifahamu Kijapani kupitia kwenye habari." Katika kipengele hiki, tunajifunza misamiati ya Kijapani kupitia habari. Kichwa cha habari cha leo ni "Njia ya kwenda kuona vivutio vya kitalii yafunguliwa tena Owakudani, Hakone", kilichowekwa kwenye tovuti ya NEWS WEB EASY Machi 29, 2022. Maneno muhimu ni pamoja na 「火山(かざん) kazan」volkano na 「お土産(おみやげ) omiyage」zawadi.