Kifahamu Kijapani
Karibu kwenye kipengele cha "Kifahamu Kijapani kupitia kwenye habari." Katika kipengele hiki, tunajifunza misamiati ya Kijapani kupitia habari. Kichwa cha habari cha leo ni "Watu nchini Japani watoa mchango wa yeni bilioni 4 kupitia ubalozi", kilichochapishwa kwenye tovuti ya NEWS WEB EASY Machi 11, 2022. Maneno muhimu ni pamoja na 「攻撃(こうげき) koogeki」 shambulio, na 「寄付(きふ) kifu」toa mchango.